2. HOMA YA DENGUE

Homa ya dengue hupatikana sana Afrika, Asia na baadhi ya maeneo ya Caribbean. pia inapatikana maeneo mengine kama marekani na maeneo yenye joto. Dengue ni katika homa ambazo ni hatari sana. kama ilivyo virusi vua Zika havina chanjo, pia hakuna chanjo ya dengue.

 

Dengue husambazwa na aina ya mbu waitwao Aedes aegypti. Mbu hawa pia wanang'ata wakati wa mchana tofauti na mbu wa Malaria. Dalili za dengue huweza kutokea siku nne mpaka saba baada ya kung'atwa na mbu.

 

Dalili za dengue dengue ni:-homa, maumivu ya kichwa, macho, viungio pamoja na misuli au miguu. Ugonjwa wa dengue mara chache hupelekea kifo. Dalili hizi zinakuwa hatari pale mgonjwa anapopata homa ya hemorrhagige. Hii hupelekea mgonjwa kutoka damu, ambayo haikati. Na hali hii pia inaweza kupelekea presha yaani shinikizo la damu kushuka sana.