DALILI ZA MALARIA

 

Dalili za malaria huenda pia zikafungamana na maradhi mengine, lakini endapo zikikusanyika pamoja kwa asilimia kubwa vitakuwa vinaonyesha uwepo wa malaria. Kumbuka hizi ni dalili tu, lakini ni vyema kupima ili kuwa na uhakika zaidi kabla ya kumeza dawwa.

 

Homa, homa ni kupanda kwa joto mwilini. Kikawaida homa ni dalili za maradhi mengi sanaila leo nitakueleza homa ya malaria ilivyo. Kikawaida hima ya malaria inaweza kuambatana na mambo kadhaa wa kadhaa. Mambo hayo ni kama


Kuhisi baridi, kutetemeka na kutaka kuotea jua ama moto. Haijalishi ni saa ngapi iwe mchana ama usiku lakini mgonjwa atahisi baridi kali sana. Na inaweza kumsababishia hali ya kutetemeka viungo ama taya za mdomo wake kugongana kwa baridi. Hivyo endapo homa itaungana na hali hii huenda ni malaria. Lakini haitishi, inaweza pia kuambatana na japo hili hap chini:-

 

Maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya misuli pamoja na viungio. Endapo homa ya mgojwa itaambatana na baridi, kisha ikafuatiwa na maumivu ya kichwa, maumivu haya yanaambatana na misuli kuuma pamoja na viungio. Mgonjwa anahisi katikati ya akutano ya viungio kama kuna vuta. Halli hizi zikikusanyika kwa pamoja huashiria malaria.

 

Mvurugiko wa tumbo unaopelekea kichefuchefu, ama kuharisha, ama kutapika ama vyote kwa pamoja. Mgonjwa anaweza kupata hali moja kati ya hizi ama akawa nazo zote. Mgonjwa anaweza kutapika maji ama chakula alichokula ama anaweza kutapika ile tunayoita nyongo. Hali hizi zinaweza kumpelekea mgonjwa akachoka sana. Tofauti na kuchoka huku lakini hatakuwa na hamu ya kula, na hata ladha ya chakula inabadilika na kuwa kichungu.

 

Uchovu, kukosa hamu ya kula, maumivu ya viungo, kuchanganyikiwa, maumivu ya kichwa, kutapika ama kuharishah. Hizi ni katika dalili za malaria.