Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles. Kuna aina zaidi ya 2000 za mbu lakini katika aina hizi aina moja tu ndio inayoweza kubeba vimelea hivi vinavyoweza kusababisha malaria. Na pia yapo maradhi mengine ambayo husambazwa na aina nyingine za mbu. Maradhi hayo ni kama matende na ngiri maji.
Mbu aliyebeba vimelea vya malaria akimng’ata mtu anamuachia vimelea vile. Vimelea hivi vinapoingia ndani ya mwili viunakimbilia kwenye ini ambapo huko ndipo hukaa na kukuwa. Pindi vikikomaa vinatoka kwenye ini na kuelekea kwenye damu. Vinapofika kwenye damu vinakwenda kushambulia seli hai nyekundu za damu. Na hapo sasa mgonjwa ndipo ataanza kupata dalili za malaria..
Inachukuwa takribani wili ama na zaidi kwa vimelea hivi kuanza kuonesha dalili kwa mtu. Pia upo uwezekano vimelea hivi vikakaa hata mwaka ndipo vikaanza kuonyesha dalili. Na ndio maana ni vyema kupima afya mara kwa mara ili kuweza kuondoa vijidudu hivi kwenye miili yetu hata kabla ya kuanza kuonyesha dalili.