Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh
Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo. Mfalme na mmiliki wa ulimwengu na siku ya mwisho. Sala na amani zimuuendee kipenzi cha Allah mtume Muhammad (s.a.w) pamoja na masahaba zake na watu wa familiya yake.
Ama baada ya utangulizi huu, hiki ni kitabu cha dua kilichoandaliwa kwa ajili ya kutoa mafunzo juu ya dua na yanayohusiana. Kitabu hiki kimeandaliwa kwa lugha ya kiswahili na iliyo nyepesi zaidi ili kuwezesha wasomaji wapate kuelewa. Maandalizi ya kitabu hiuki yametokana na mafunzo kutoka kwenye quran na sunnah.
Kitabu hiki ni waqfu kwa ajili ya Allah na hakiuzwi. Kwa yeyote atakayetaka kukiprint awasiliane nasi kwa 0620555380 au admin@bongoclass.com. Kitabu hiki kimeanza kusambazwa kwa njia ya kimtandao hivyo tunatoa wito kwa anayeteka kukiprint awasiliane nasi kwa haraka zaidi.
Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo huu wa vitabu vya dua kutoka kwetu. Inshaa Allah tunatarajia kutoa mwendelezo wa kitabu hiki siku za mbeleni. Pia tunatoa wito kwa yeyote mwenye kuweza kuandika vitabu awasiliane nasi lkwa ajili ya mazungumzo zaidi.
Tumeandaa kazi hii kwa ajili ya Allah kwa kutaraji radhi zake na si vinginevyo. Pia tunatarajia dua kutoka kwenu wasomaji ili Allah atusamehe madhambi yetu pamoja na wazazi wetu na waislamu kwa ujumla.
Tunaomba kwa yeyote atakayeona kuna makosa kwenye kitabu hiki awahi haraka sana kuwasiliana nasi ili kuzuia kusambaa kwa makosa zaidi. Kitabu hiki cha kwanza nimekigawa katika sehemu kuu tano kama zitakavyoelezwa chini hapo.
Wabillah tawfiq
Al- ustadhi Rajabu Athuman
0620555380
admin@bongoclass.com