VYAKULA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

VYAKULA

YANAYOATHIRI AFYA
Afya yamtu inaweza kuathiriwa kuwa njema au kuwa mbovu kwa kuzingatia mambo kadhaa wakadhaa. Hapa nimechagua mambo makuu matano ambayo nitakwenda kuyaangalia ambayo ni;-
A).vyakula
B)Mazingira
C)Shughuli za kila siku
D)Tabia na mazoea
E)Vizazi, familia ama kurithi.
1.VYAKULA
Vyakula ni katika sababu kubwa ambazo husaidia kwa kiwango kikubwa kuathiri afya za watu. Wataalamu wa afya leo wanaeleza na kutaja magonjwa mengi sana ambayoyo yanapatikana kwa kupitia vyakula. Pia yapo magonjwa ambayo huambukizwa kwa kupitia ulaji wa chakula. Hivyo magonjwa mengi na hatari zaidi yamekuwa na mahusiano na vyakula vyetu. Chakula kinaweza kuwa msaada kwako au kuwa ni chanzo cha matatizo ya afya yako. Mfano mzuri ni kuwa leo wataalamu wa afya anaeleza kuwa mamilioni ya watu wanakufa kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka. Tafiti zinaonesha kuwa miongoni mwa sababu za ugonjwa huu ni vyakula. Vyakula ambavyo tunavila leo sio rafiki kwa afya zetu. Tumekuwa tukila vyakula ambavyo vimejaa kemikali nyingi na matatizo kadha wakadha.

Mfano wa pili ni ugonjwa wa kisukari, huu ugonjwa umekuwa ukienea kwa kasi sana duniani leo. Kuanzia watoto, vijana wazee na wajawazito wote wapo hatarini kuapata maradhi haya. Wataalamu wa afya wanataja kuwa vyakula ni katika sababu mjawapo ya kupata maradhi haya. Kuongezeka kwa uzito nje ya uzito wa kawaidi ni katika sababu za kutokea kwa kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula ni sababu ya kuongezeka kwa uzito mwilini na kutofanya mazoezi ijapokuwa zipo sababu zingine.

Magonjwa ya moyo kama shinikizo la damu (presha) pamoja na shambulio la moyo (heart attack) ni katika magonjwa yanayowapata watu weng duniani na kusababisha vifo vingi sana. Wataalamu wa afya wanaeleza katika sababu kubwa za kutokea kwa maradhi haya ni vyakula. Hususan vyakula vyenye mchanganyiko mkubwa wa mafuta ya viwandani.

Maradhi ya utapiamlo kama matege, baadhi ya matatizo ya macho, unyafuzi na kwashiakoo pamoja na kudumaa ni katika maradhi ambayo husababishwa na vyakula. Majeraha kutokupona haraka, kuchelewa kupona kwa vidonda na makovu, ngozi kupasuka na kutokwa na vidonda kwenye mdomo ni katika baadhi ya matatizo yanayosababishwa na vyakula Kwa ufupi ni kuwa vyakula ni katika sababu kubwa sana ya maradhia mabayo tuanayapata. Tutazungumzia kwa undani zaidi somo hili kwenye kurasa zijazo na tutaona kwa undani vipi vyakula vinaweza kusababisha yote hayo.


                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 77

Post zifazofanana:-

hukumu ya ombaomba katika uchumi wa kiislamu
Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili. Soma Zaidi...

ZIJUWE NYANJA KUU 6 ZA AFYA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Korodan kuwasha ni mja ya dalil ya fangas ,na ulimi kuchanka pmja na maumivu ndan ya mdomo wa juu na chini
Swali langu. Soma Zaidi...

MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...

Faida za kula Zaituni
Matunda ya zamani, matunda ya asili, Zaituni tunda lipendezalo, zijuwe faida zake leo Soma Zaidi...

Kupanga uzazi na uzazi wa mpango katika uislamu
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al-Falaq na surat an-Nas na fadhila za kusoma sura hizi
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Kuepuka mabishano na madhara ya kugombana
16. Soma Zaidi...

NDOA YA SINBAD NA BINTI WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME. Soma Zaidi...

Nini maana ya riba, na yapi madhara yake?
8. Soma Zaidi...

Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Hii ndio namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume s.a.w
Mtume (s. Soma Zaidi...