1.MAGONJWA YA MOYO:
Moyo unanasibiana na magonjwa mengi sana ambayo wengi hawayajui. Watu wamezoea presha kuwa ndio gonjwa la moyo wanalolijua, ila sio hivyo kuna mengi zaidi. Hali za maisha zinaweza kuwa sababu nzuru ya kupata magonjwa ya moyo, miongoni mwa hali hizo ni kutofanya mazoezi ama vyakula mtu anavyokula

Cardiovascular diseases (CVD) ni maradhi au upungufu flani unaotokea kwenye moyo au mishipa ya damu. Moyo na mishipa ya damu hutengeneza mfumo unaoitwa cardiacvascular system. Hivyo magonjwa yote na matatizo yeyote yanayotokea kwa kuathiri moyo na mishipa ya damu huitwa magonjwa ya cardiacvascular diseases. Tafiti zilizofanywa marekani zinaonesha kuwa maradhi haya ndio yanayochangia vifo vya watu wengi marekani. Miongoni mwa magonjwa haya ni kama shambulio la moyo (heart attact), kupalalaiz (stroke), shinikizo la juu la damu yaani presha ya kupanda na atherosclerosis. Magonjwa haya hushambulia zaidi watu walio na umri zaidi di ya miaka 40. Na maradhi haya yanaweza kutokea tangia utototni.

Unawezakupata maradhi haya kwa kurithi kutoka kwa wazazi, ila inategemea namna unavyoishi ndio tatizo linaweza kuwa kubwa ama dogo. Kwa mfano kuvuta sigara, kuwa na uzito mkubwa, kuwa na kisukari na kuwa na cholesterol nyingi kwenye damu husababisha tatizo hili kuwa kubwa zaidi. Tafiti zinaonesha karibia milioni 60 marekana wana moja kati ya magonjwa hya na karibia watu milioni moja hufa kwa sababu ya magonjwa haya kila mwaka.

AINA ZA MAGOJWA HAYA (CARDIACVASCULAR DISEASES)
1.Kupalalaizi (stroke); karibia watu 160,000 hufa kwa stroke. Stroke ni shambulio la harka amablo linatokea pindi damu inayotembea kwenye ubongo ikapata hitilafu yoyote. Hutokea pindi damu ikaganda katika vimishipa hivyo na kuzuia mzunguruko wa damu kwenye ubongo. Au hutokea mishipa ikapasuka na kusababisha damu kuvuja kwenye ubongo. Hali hizi zote zikitokea hueza kusababisha kupalalaizi. Mishipa hii huweza kupasuka kama shinikizo la damu likawa kubwa sana. Wataalamu wa afya wanatueleza dalili ya tatizo hili kabla halijatokea. Dalili hizi ni kama:-
A).Kuchoka kwa ghafla kwa mikono, miguuna kuona maluelue.
B).Kushindwa kuona jicho moja au yote
C).Kizunguzungu cha ghafla au kupoteza fahamu.
D).maumivu ya kichwa ya ghafla bila ya sababu maalum

2.Shinikizo la juu la damu (high blood pressure);Kitaalamu tatizo hili huitwa high blood pressure au hypertension. Watu wengi hawajijui kama wana tatizo hili ila wanakuja kujikuta wamepatwa na shambulizi la moyo (heart attack) au stroke. Shinikizo la damu ni hali inayotokea katika mfumo wa damu ambapo kasi ya mzunguruko wa damu inakuwa kubwa zaidi kiasi kwamba njia haitoshi hivo kujalibu kutanua kuta za mishipa ya damu na misuli ya moyo

. Huweza kusababisha stroke au kuufanya moyo kufanya kazi kwa taabu ama moyo kushindwa kabisa kufanya kazi. Pia huweza kuathiri baadhi ya viungo vya mwili kama figo, na macho. Kuganda kwa mafuta kwenye kuta za damu huenda ikawa ni sabubu kubwa ya kutokea kwa tatizo hili kama tutakavoona hapo mbele.
v 3.Shambulio la moyo (heart attack); mishipa ya coronary arterries inakazi ya kusafirisha dabu yenye oxyjen na virutubisho (nutrients) kwa ajili ya kulisha seli za moyo zinazoufanya moyo ufanye kazi yake. Mishipa hii ni myembamba na imeuzungurika moyo.sasa ikitokea damu imeganda kwenye mmoja ya mishipa hii na kuzuia damu isipite kwenye mshipa ule na kuifanya damu isifike kwenye moyo, hii huweza kusababisha seli za moyo zikafa kwa kukosa hewa ya oksijeni na virututisho vilivyotakiwa kuletwa kupitia mshipa ule.

Na hapa mtu atasikia maumivu kwenye kifua chake. Na hii ni kwa sababu ya moyokutoweza kupata damu ya kutosha. Shambulio la moyo ni kuathirika kwa misuli ya moyo au kushindwa kufanya kazi misuli ya moyo. Shambulio la moyo halinaga dalili za waziwazi ila wataalamu wa afya wanataja hizi;-
A)kuhisi kubanwa na maumivu katikati ya kifua na hali hii huendelea kwa muda wa dakika kadhaa.
B)Maumivu yanayoendelea mpaka kwenye mabega, shingo na mkono.
C)Kutokujisikia saswa kifuani kunakofuatana na kuzimia, kutoka jasho jingi sana, damu za pua, au kuvuta punzi chache sana.

4.Atherosclerosis; hii hutokea pale mishipa ya damu inapokuwa na mafuta (fatty) yaliyoganda kwenye mishipa hiyo na kuathiri mzunguruko wa damu wa kawaida. Hali hii ni hatazi kwani inaweza kuzuia damu kuzunguruka katika shemu kadhaa za damu. Pia kama donge la mafuta haya likibanduka na kuingiea kwenye damu na likaingia kwenye coronary arterries (vimishipa vinavyolisha misuli ya moyo) inaweza kusababisha shambulio la moyo na kama litaingia kwenye ubongo litasababisha stroke. mafuta Kawaida

NAMNA YA KUPAMBANA NA MARADHI HAYA
1.Punguza kula kula vyakula vya mafuta kwa wingi na upunguze pia kula chumvi nyingi.
2.Hakikisha uzito wako upo katika kiwango kinachotakiwa. Nnda kapime ujuwe unazito sahihi.
3.Wacha kuvuta sigara
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Punguza misongo ya mawazo.