2.TAHADHARI KWENYE MAZINGIRA
Kama tulivyoona hapo juu, mazingira yetu ni sababu tosha ya kuathiri ubora wa afya zetu. Hivyo mtu ahakikishe sikuzote anaishi katika mazingira salama na safi. Wataalamu wa afya wanatueleza kusafisha mazingira yetu ya ilasiku ili tuweze kukabilia na na wadudu hatara.

Hakikisha hewa unayoipata ni safi na salama. Futa mavumbi ndani ya nyumba na nguo za kujifunika ziwe safi, kwa namna hii ni rahisi kukabilia na na mafua. Epuka moshi kutoka viwandani, pia usilale ukiwa na jiko la mkaa linalowaka na ikawa madirisha na milango umefunga. Unaweza kupata tatizo la kukosa oxkyjeni na kufariki dunia. Kaa mbali na wavuta sigara kwani hewa yao inaweza kukuathiri na wewe pia. Jambo la msingi hapa ni kuchukua tahadhari dhidi ya hewa ambayo tunaipata kwenye mazingira hetu.

Hakikisha unafyeka na kupunguza nyasi zilizo karibu na wewe. Fukia madimbwi na majimaji yoyote yalotuwama hata kama yapo kwenye kifuniko cha soda kwani hayo ni machache lakini mamia ya mbu yanaweza kuzaliana hapo. Mashimo ya kutupia taka yawe mbali kidogo na nyumba na kuwepo utaratibu wa kuchoma moto mashimo hayo bada ya muda. Usafi wa mazingira unaweza kuwa njia tosha ya kuanza harakati za kukabiliana na malaria na kipindupindu.

Watu wahakikishe wanakunywa maji safi na salama pamoja na kula vyakula ambavyo vimehifadhiwa kwa usalama. Usafi wa maji unaweza kuwa njia ya kupambana na typhod (taifodi) na maradhi mengine ya tumbo. Kuwepo na utaratibu wa kuyatibu maji kama yamepatikana sehemu ambazo sio salama na safi. Maji yanaweza kutibiwa kwa njia za kisasa kama kuweka madawa. Lakini pia unaweza kutumia njia ya kuyachemsha na kuyachuja na kuyatumia.

Sikuzote hakikisha unaishi katika mazingira rafiki na afya yako. Watu ambao tayari wanamaambukizi ya maradhi maalumu wanatakiwa waishi katika mazingira ambayo ni rafiki na hali zao.