Dalili za HIV na UKIMWI kwenye Ulimi na Mdomo

Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi utaziomna hapa. hizi zinaweza kuwa ndio za kwanza kwa ambaye hajapima HIV

Dalili za HIV na UKIMWI kwenye Ulimi na Mdomo


DALILI ZA UKIMWI NA HIV KWENYE ULIMU NA MDOMO


HIV hivi ni virusi vilivyopata umaarufu sana kwa kufahamika kuwa ndio virusi pekee vinavyoweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI. Virusi hivi anaweza kuvipata binadamu yeyote yule. Zipo njia nyingi ambazo unaweza kupata virusi hivi kama kushiriki ngono zembe, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kijifungua, kushiriki vitu vyenye ncha kali, kupewa damu yenye virusi, na njia nyingine kibao. Dalili za HIV na UKIMWI zinatofautiana kulingana na hatua ya mgonjwa. Lanini kuna wakati Ulimi na Mdomo kuweza kuonyesha dalili hizi wazi wazi.


Dalili za HIV na UKIMWI kupitia mdomoni zinaweza kuwa ni dalili za mwanzoni sana za UKIMWI kwa baadhi ya watu. Ukweli ni kuwa dalili hizi zinaweza kumpata yeyote lakini kuna watu wapo hatarini zaidi kama watoto wachanga, wazee na watu wenye upungufu wa kinga yaani UKIMWI. Dalili hizi tutaziona moja hadi nyingine hapo chini.


Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi
1.Kukauka kwa mdomo na kuoza kwa meno.
Virusi vya HIV vinaweza kupelekea mdomo kukauka na kukosa mate ya kutosha. Hivyo miongoni mwa kazi za mate ni kulinda meno na mdomo. Hivyo kupelekea meno kuoza. Ni vyema mgonjwa kama anatatizo hili kuonana na daktari aweze kumpa ushauri. Unaweza kutumia dawa maalumu kwa ajili ya kuchochea mate ama kutafuna bigji ambazo hazina sukari.


2.Kupata fangasi wa kwenye mdomo wajulikanao kama candidiasis (thrush).
Fangasi hawa wanaweza kusababisha madoa mekundu kwenye ulimi, ama mdoa meupe kwenye mdomo. Pia wanaweza kusababisha kupasuka kwa kona za mdomo na kutengeneza weupe kwenye kona za mdomo. Pia mdomoni kunaweza kuta buda la nyama lisilokuwa na maumivu. Fangasi hawa wanaweza kuhamia kwenye koo na kusababisha maumivu. Fangasi hawa ni rahisi sana kuondoka baada ya matibabu ila kwa baadhi ya sababu wanaweza kuwa sugu.


3.Vidonda kwenye mdomo na ulimi
Hivi ni vijidonda vijidogo ambavyo vipo duara. Vinaweza kutokea kwenye ulimi na kwenye mashavu kwa ndani. Pia vinaweza kutokea nyuma ya koo. Vidonda hivi vinakuwa na rangi nyekunu pembeni na rangi ya kijivu katikati. Misongo ya mawzo na baadhi ya vyakula vinaweza kuwa ni sababu.


4.Vidonda vya homa.
Kama umeshawahi kushuhudia vidonda ambavyo vinatokana na homa. Vidonda hivi kwa watu wenye UKIMWI vina tabia ya kujirudia mara kwa mara. Dawa za ART huweza kusaidia hali hii kutotokea.


5.Maradhi ya ufinzi ama periodontitis or gingivitis
Haya ni maradhi ya ufizi ambapo ufinzi unakosa nguvu na kushindwa kuzuia meno vyema. Hal hii inaweza kupelekea kung'oka kwa meno. Hali hii inaweza tokea mapema sana miezi 18 baada ya kupata HIV. Ukavu kwenye mdomo, kuvuta sigara kunaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.


6.Kuota kwa kambakamba ama vinywele vinywele kwenye ulimi na pembeni ya ulimi.
Kitaalamu hivi hujulikana kama Hairy Leukoplakia. Vikambakamba ama vinyweleo nyweleo hivi havina maumivu lakini pia haviwezi kutoka hata kwa kupiga mswaki. Hii inaweza kuwa ni katika dalili za mwanzo zaidi za UKIMWI. Vyenyewe vipo na rangi nyeupe


7.Madoa ya rangi ya dhambarau iliyowiva ama nyekundu kwenye mafinzi, sehemu ya juu ya mdomo na nyuma ya ulimi. Kitaalamu hufahamika kama Kaposi's Sarcoma (KS Hii inaweza kuwa ni dalili ya kwanza kwa mtu ambaye hajapima HIV. Na kwa ambaye ameshaanza kutumia dawa dalili hizi ni si rahisi kujionyesha.


8.Kuota chunjua kwenye mdomo,na ulimi. Hizi husababishwa na virusi vinavyojulikana kama Human Papillomavirus, HPV. Kikawaida chunjua inaweza kuota popote pale kwenye mwili hasa hasa hutokea mara nyingi kwenye mikono. Watu wenye HIV chunjia hizi huweza kuvamia ulimi na kuhama maeneo mengine kwenye mdomo. Pia baadhi ya virusi wanao;eta hali hii wanaweza kusababisha saratani.


Mwisho nikufahamishe tu kuwa mdomo ni katika sehemu za kwanza kuonyesha dalili za HIV na UKIMWI. Ni vyema kwenda kupima endapo utagundua una moja ya dalili hizo hapo juu.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2073

Post zifazofanana:-

viapo
20. Soma Zaidi...

Naman ya kuiendea quran na kuifanyia kazi baada ya kuisoma
Soma Zaidi...

KITABU CHA AFYA (kisukari, saratani, vidonda vya tumbo, HIV na UKIMWI) DALILI NA CHANZO
Soma Zaidi...

Ni ipi siku ya kupata ujauzito, na nitajuwaje kama nimepata ujauzito?
Hapa utajifunza siku nzuri kushoriki tendo la ndoa kupata ujauzito, dalili za siku hiyo na kuitafuta kwa mahesabu Soma Zaidi...

v
Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake. Soma Zaidi...

ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli
Ukweli ni uhakika wa jambo. Soma Zaidi...

Taasisi za Kifedha Katika Mfumo wa Uchumi wa Kiislamu
- Ni taasisi za kifedha zinazohusika na kuhifadhi akiba na mali za watu zenye thamani kubwa kama dhahabu, n. Soma Zaidi...

CANCER FIGHTING FOODS
Cancer fihting foods Cancer is in the world's most common serious illnesses. Soma Zaidi...

tarekh
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...

Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Soma Zaidi...

Ulaji wa protini unasaidia kupunguza unene
Soma Zaidi...

nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...