Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa

Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii

Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa


MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA NA BAADA



Hii ni hali inayowapata wanawake kwa kiasi kikubwa wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Maumivu haya pia yanaweza kumpata mwanaume ila kwa uchache sana. Hali hii kitaalamu inafahamika kama dyspareunia.


Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa uume unapoingia kwa mara ya kwanza, ama wakati wote wa kuingia na kutoka ama baada ya kumaliza tendo la ndoa. Maumivu ya wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwenye uke, ama uume ama kwenye tumbo kwa kwa wanawake. Makala hii itakwenda kukuorodheshea sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa.


Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
1.Uke kuwa mkavu kutokana na maandalizi mabovu kabla ya kuingiza uume. Pia inaweza kuwa ni kutokana na kukosa hamu ya kushiriki tendo.


2.Kuwepo kwa majeraha kwenye uume ama uke. Majeraha haya yanaweza kuwa ni kukeketwa ana ya namna nyingine.


3.Kuwepo kwa uvimbe ama ukawa na matatizo ya ngozi katika sehemu za siri. Haya yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kuingia kwa uume.


4.Maumbile ya uke. Wakati mwingine jinsi uke ulivyo inaweza kuwa ni tatizo. Kuwa uke mwingine unatabia ya kubana misui yake. Hali hii inaweza kupelekea maumivu wakai wa kupenya kwa uume.


5.Matatizo ya kimaumbile, kwa mfano kuwa na ukilema kwenye uke, ama kuwa na nyama ama ngozi ambayo inaweza kuzuia kupenya kwa uume.


6.Kuwepo kwa maradhi katka mfumo wa uzazi wa kike. Matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwa kwenye ovari, ama kukawa na uvimbe ndani ya kizazi ama kukawa na shida katika mirija ya uretas.


7.Kufanyiwa baadhi ya matibabu katika maeneo ya siri. Kwa mfano baadhi ya matibabu ya saratani katika sehemu za siri, matibabu haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa


8.Matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawaso. Wakati mwingine uoga, kuwa na msongo wa mawazo ama kukumbuka maumivu uliyoyappata siku zanyuma, hali hizi zinaweza kupelekea maumivu wakati mwingine.


9.Staili iliyotumika wakati wa kufanya sex. Wakati mwingine mikao ya kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa ni sababu ya maumivu. Ni vyema kutumia mikao iliyo rahisi.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 257


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-