Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)

Historia ya kuhifadhiwa na kuandikwa kwa quran toka wakati wa Mtume (s.a.w)

Kuhifadhiwa kwa Qur-an



Tofauti na vitabu vingine vya Allah (s.w) vilivyotangulia, Qur-an ina ahadi ya Allah (s.w) ya kuhifadhiwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


"Hakika sisi ndio tulioteremsha mawaidha haya (hii Qur-an) na hakika sisi ndio tutakaoyalinda". (15:9)


"Haitakifikia batili mbele yake wala nyuma yake, kimeteremshwa na Mwenye Hikima ahimidiwaye." (41:42)
Kutokana na aya hizi, Qur-an iko vile vile kama ilivyoteremshwa na haijabadilika hata kidogo. Kila aya zilivyoshuka zilihifadhiwa kwa njia tatu zifuatazo:



Kwanza, alihifadhishwa Mtume (s.a.w) na kuahidiwa na Mola wake kuwa hatasahau kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:



"Tutakusomesha wala hutasahau ila akipenda Mwenyezi Mungu. Yeye anajua yaliyodhahiri na yaliyofichikana." (87:6-7)


"Usitikise ulimi wako kwa (kuufanyia haraka) wahyi. Kwa hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. Wakati tunapokusomea basi fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu yetu kuubainisha." (75:16-1 9)



Pili, Waislamu walihifadhi Qur-an vifuani mwao baada ya kusomewa na Mtume (s.a.w).



Tatu, Qur-an ilihifadhiwa katika maandishi chini ya usimamizi wa Mtume (s.a.w) mwenyewe. Kila aya ya Qur-an iliposhuka iliandikwa wakati ule ule katika karatasi maalumu za ngozi (Qur-an 52:3) na waandishi wa Mtume (s.a.w) chini ya uangalizi na usimamizi wake kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:



Uthman bin Afan (r.a) amesimulia: "Wakati wowote Mtume wa Allah alipoteremshiwa wahyi humuita mmoja wa watu waliochaguliwa kuandika." (Tirmidh)



Naye Zaid bin Thabit mmoja wa waandishi wa Qur-an anasema: "Nilikuwa jirani na Mtume wa Allah, kwa hiyo kila alipoteremshiwa wahyi ilikuwa kawaida yake kuniita nami niliandika aliyoniamuru." (Abu Daud)


Idadi ya waandishi wa Qur-an aliowateua Mtume (s.a.w) ilifikia hadi 42. Miongoni mwa waandishi wa Mtume (s.a.w) ni pamoja na Makhalifa wake wanne - Abu bakr, Umar, 'Uthman na Ally (r.a). Waandishi wengine waliokuwa mashuhuri ni Zaid bin Thabit, Abdullah bin Mas-'ud, Ubayyi bin Ka'ab, na Khalid bin Walid.



Mtume (s.a.w) baada ya kuwaamuru waandishi wake wa Qur-an waandike kile alichowasomea, pia aliwaamuru wamsomee walichoandika na alifanya marekebisho pale walipokosea kama tu navyoj ifu nza katika had ith ifuatayo:



Zaidi bin Thabit amesema: "' Kila nilipomaliza kuandika (Wahyi) Mtume aliniamuru nisome nilichoandika na nilikuwa ninamsomea. Kama palikuwa na kosa alilisahihisha kisha aliwapa watu (kunakili na kuhifadhi vifuani).



Pia Mtume (s.a.w) ndiye aliyewaelekeza waandishi wake wa Qur-an wazipange aya na sura kama zilivyo katika msahafu tulionao hivi leo kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



'Uthman bin Afan (r.a) ameeleza: "Ilikuwa kawaida ya Mtume wa Allah kila aliposhushiwa aya za sura mbali mbali (za Qur-an) au kila aya iliposhuka alimuita mmoja wapo wa waandishi wa Qur-an na kumwambia, "Andika aya hizi katika Sura kadhaa baada ya aya kadhaa."



Pamoja na Hadithi hii kuna hoja kadhaa za kihistoria zinazothibitisha kuwa Qur-an iliandikwa na kukusanywa katika msahafu tulionao hivi leo chini ya usimamizi na uangalizi wa Mtume (s.a.w) mwenyewe. Baadhi ya hoja hizo ni hizi zifuatazo:



Kwanza Anas (r.a) aliyekuwa miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w) ameeleza kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) aliwaamuru waigawanye Qur-an katika mafungu saba baada ya Suratul-Fatiha (sura ya ufunguzi). Fungu la kwanza katika haya lilikuwa na sura tatu, kisha likafuatiwa na fungu la sura tano, kisha la sura saba, kisha la sura tisa, kisha la sura kumi na moja, kisha la sura kumi na tatu na mwishowe sura zote zilizobakia ziliwekwa katika fungu moja. Fungu hili la mwisho limeanza na Suratul Qaaf. Ukihesabu sura zote pamoja na sura ya ufunguzi (Suratul-Fatiha) utakuta Suratul-Qaaf inakuwa ni sura ya hamsini (50). Sura hii pia ni ya 50 katika Msahafu tulionao hivi leo kuthibitisha kuwa mpango wa sura katika msahafu ulioelekezwa na Mtume Muhammad (s.a.w) haujabadilika mpaka hivi leo.



Pili Katika Hadithi ya Abu Daud, Hudhaifa (r.a) anasimulia kuwa amemuona Mtume (s.a.w) akisoma sura ya Al-Baqara, Al-Imran, An-Nisaa,Al-Maida na Al-An-'am katika mfuatano huo. Mpango wa sura hizi kama zilivyotajwa katika Hadithi hii ni kama ziivyo kwenye msahafu baada ya sura ya ufunguzi ambayo pia imebakia sura ya kwanza katika msahafu tangu alivyoiweka Mtume(s.a.w) katika nafasi ilipo. Hii inaonesha kuwa mpango wa sura lazima uwe umepangwa na Mtume(saw) mwenyewe kama alivyoongozwa na Allah (s.w).



Tatu Imam Tirmidh katika kitabu chake cha Hadithi anatufahamisha hadithi ifuatayo:
"Mtu mmoja aliuliza: "Ewe Mtume wa Allah! Tendo lipi ambalo Allah hulipenda kuliko yote?" Akajibu (Mtume) ("Tendo) la yule amalizaye safari na kisha akaendelea nayo". Pakaulizwa: "Nini maana ya kumaliza safari na kuanza nyingine?" Mtume alijibu: "Mwenye kuisoma Qur-an anaisoma tangu mwanzo hadi mwisho na amalizapo anarudia mwanzo na kusoma tena hadi mwisho na hufanya hivi kuwa kawaida yake; yaani kila amalizapo anaanza upya" (Darmi). Suala la kusoma Qur-an tangu mwanzo hadi mwisho ni hoja tosha ya kuwepo kwa mpango wa sura ya kwanza hadi mwisho.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1701

Post zifazofanana:-

TAMBUA NAMNA YA KUTOA HUDUMA YA KWANZA WAKATI WA DHARURA, AJALI NA HATARI
Soma Zaidi...

Harun(a.s), Achaguliwa Kuwa Msaidizi Musa(a.s) na kumkabili (kumlingania) firauni
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

bongoclass health
1. Soma Zaidi...

Maudhui ya Qur-an na Mvuto wa Ujumbe Wake
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUPASULIWA KWA KIFUA AU TUMBO CHA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) AKIWA MTOTO KWA BI HALIMA
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO. Soma Zaidi...

nina maambukizi ya zinaha maumivu wakati wa kukojoa na usaha
Mimi nilifanya ngono isiyo salama Tar 14/07 mwaka huu, nilikutana tu na mwanamke ambae sikuwa hata na background yake yoyote hivyo baada ya siku tatu nilijikuta nina maambukizi ya zinaha (maumivu wakati wa kukojoa na usaha), hivyo nilienda hospital na kup Soma Zaidi...

Vyakula vyenye vitamini C kwa wingi
Vitamini C kwa wingi hupatikana kwenye machungwa, maembe, mananasi, limao na ndimu Soma Zaidi...

VYNZO VYA MINYOO: nyama isiyowiva, maji machafu, kinyesi, uchafu wa mazingira, udongo
VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao. Soma Zaidi...

tarekh 02
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake
Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s. Soma Zaidi...

VIPI VIDONDA VYA TUMBO VINATOKEA
VIPI VIDONDA VYA TUMBO VINATOKEA 1. Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...