Kwa nini lengo la kutoa zaka halifikiwi na watoaji zaka?

Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?

Kwa nini lengo la kutoa zaka halifikiwi na watoaji zaka?

Kwa nini Lengo la Zakat na Sadaqat Halijafikiwa katika Jamii yetu?



Tumejifunza kuwa jamii yenye kudumisha nguzo ya Zakat na kutilia mkazo suala la kutoa mali na huduma kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni jamii yenye kuendelea kiuchumi na yenye kuishi kwa furaha na amanai ya kweli ya kibinafsi na kijamii. Jamii ya Mtume (s.a.w) na ile ya Makhalifa waongofu ni mfano wa wazi ulio mbele yetu. Jamii yetu hivi leo, pamoja na mahimizo ya utoaji wa Zakat na Sadaqat katika majukwaa mbali mbali bado hatuyapati matunda ya Zakat katika jamii. Miongoni mwa sababu zinazowafanya Waislamu wasipate matunda yanayotarajiwa kutokana na utoaji wa Zakat na Sadaqat ni:



(i)Wengi miongoni mwa Waislamu Hawatekelezi Nguzo ya Zakat



Wengi miongoni mwa Waislamu wenye uwezo wa kutoa zakat hawaitekelezi nguzo ya zakat na hawajihimizi kutoa misaada midogo na mikubwa kwa wale wanaohitajia.
Kwa sababu ya kutotoa Zakat na Sadaqat kwa wale wenye uwezo miongoni mwa Waislamu, kumeipelekea jamii ya Waislamu kuwa duni na dhalili mbele aya Makafiri na Washirikina.



(ii)Wengi Watoa Zakat na Sadaqat Hawatekelezi Masharti ya Utoaji



Miongoni mwa matajiri wachache wanaojitahidi kutekeleza nguzo ya Zakat na utoaji mali kwa ajili ya kuwasaidia wanaohitajia, hawazingatii masharti ya utoaji.Baadhi ya matajiri hutoa mali zao kwa ria na hufuatilia kwa masimbulizi. Utoaji wa namna hii umefutiwa baraka na hauwezi kumnufaisha mwenye kutoa wala jamii. Ubaya wa kutoa mali au msaada wowote kwa ria na kwa masimbulizi umedhihirishwa wazi katika aya ifu atayo:



Enyi mlioamini! Msiharibu sadaka zenu kwa masimbulizi na udhia; kama yule anayetoa mali yake kwa kuwaonesha watu, wala hamwamini Mwenyezi Mungu wala siku ya mwisho. Basi hali yake ni kama hali ya jabali ambalo juu yake pana udongo, kisha ikalifikia (jabali hili) mvua kubwa (likasukuma udongo wote huo) na ikaliacha tupu. Basi haw atakuw a na uw ezo (wa kupata) chochote katika walivyovichuma; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu makafiri'. (2:264)



Kuna baadhi ya miongoni mwa Waislamu matajiri wanaotoa Zakat bila ya kuzingatia wale wanaostahiki (Rejea Qur-an, 9:60). Badala yake huenda na kapu la fedha msikitini na kumgawia kila mtu atakayekuwa tayari kupokea. Ugawanyaji huu wa Zakat hupelekea kupewa wasiostahiki na kuwakosesha wanaostahiki na kuwabakisha katika dhiki yao. Utoaji wa namna hii huibakisha jamii ya Waislamu katika dhiki na katika uadui na uhasama. Kuna baadhi ya Waislamu pamoja na kutoa Zakat na Sadaqat, hawazingatii mipaka ya halali na haramu katika uchumi wao. Wengine huchuma kwa njia za haramu ambazo hazinufaishi jamii bali huiingiza jamii katika matatizo ya rushwa, riba, kamari, wizi, ujambazi na udhalimu wa kila namna.



(iii) Zakat haikusanywi na Kugawanywa Kijamii
Tumejifunza kuwa utoaji na ugawaji wa Zakat, ili unufaishe jamii hauna budi kusimamiwa na jamii. Lazima jamii ya Kiislamu iwe na watu maalum wanaopita kwa kila Muislamu mwenye uwezo wa kutoa zakat, na kuipokea Zakat yake kisha kuikabidhi kwa Mtunzaji wa Baitil-Mali (Mhazini), kisha kuigawa kwa wanaostahiki.
Sehemu kubwa ya jamii ya Waislamu hivi leo, haifuati utaratibu huu wa ukusanyaji na ugawaji wa Zakat na sadaqat bali kila mwenye kutoa Zakat huigawanya mwenyewe kwa wale wanaostahiki walio machoni mwake. Kuacha Zakat mikononi mwa watoaji binafsi, kuna hasara kubwa zifuatazo:



Kwanza; hapitiwi na mhimizo wa makusudi juu ya utoaji wa Zaka, kiasi kwamba wenye kustahiki kutoa Zakat hujisahau na hatimaye kuacha kutoa Zakat kabisa.



Pili; kwa kutokuwa na utaratibu wa ugawaji, sehemu kubwa ya Zakat hupewa wasiostahiki na wale wanaostahiki hubaki na dhiki yao.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 382


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kifo cha Khalia Uthman kilivyotokea
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

Sababu nyengine zilopelekea kushushwa kwa suratul ikhlas
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Upinzani Dhidi ya Ujumbe wa Mtume(s.a.w)
Mtume(s. Soma Zaidi...

DUA 51 - 60
51. Soma Zaidi...

Ni mambo yapi hupunguza Swawabu na malipo yamwenye kufunga
Soma Zaidi...

Taathira ya Imani ya Malaika katika maisha ya kila siku
Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini. Soma Zaidi...

Jinsi Mtume Muhammad (s.a.w) alivyoipokea Qur-an:
(iii)Jinsi Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

Namna ya kutufu, na masharti ya mwenye kutufu
3. Soma Zaidi...

HIKUMU YA BASMALLAH YAANI KUSOMA BISMILLAH
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...