Ni mambo yapi hupunguza Swawabu na malipo yamwenye kufunga

Ni mambo yapi hupunguza Dhawabu na malipo yamwenye kufunga

Yanayoharibu au Kupunguza Thamani ya Funga


Yanayoharibu funga ya mtu au kupunguza thamani yake ni kujiingiza katika mazungumzo yaliyokatazwa kama vile kusengenya, kusema uwongo, kupiga porojo, n.k., na kujiingiza katika matendo maovu. Japo mtu mwenye kufanya matendo haya atajiona amefunga kwa vile atakuwa hajala, au hajanywa au hajafanya kitendo chochote katika vile vinavyobadtilisha funga atakuwa hana funga au hakupata malipo ya funga kwa ushahidi wa Hadith ifuatayo:


Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Yoyote yule ambaye hataacha mazungumzo mabaya na vitendo viovu, Allah (s.w) hana haja na kuacha kwake chakula chake na kinywaji chake (Allah (s.w) hatapokea funga yake). (Bukhari).


Wakati mmoja Mtume (s.a.w) aliwaamuru watu wawili wafuturu (wavunje funga) kwa sababu walikuwa wanasengenya.
Wanachuoni wameshindwa kutoa uamuzi kuwa mtu akizungumza maneno maovu na machafu au akijiingiza katika matendo maovu, atakuwa amefungua kwa sababu ni vigumu kujua matendo ya ndani ya mtu. Hivyo, japo hapatakuwa na mtu yeyote atakayekuambia umefungua kwa kufanya vitendo viovu, wewe mwenyewe ujihesabu kuwa hukupata kitu kutokana na funga yako kama Mtume (s.a.w) anavyotufahamisha katika hadith ifuatayo:


'Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Ni watu wangapi wanaofunga, lakini hawana funga ila huambulia kiutu ...' (Darimi).
Mfungaji anatakiwa, ili funga yake iweze kutimia na kufikia lengo, ajiepushe na mambo yote maovu na machafu. hata akichokozwa na mtu, ajiepushe kugombana naye kwa kumwambia, 'Nimefunga, nimefunga' kama anavyotushauri Mtume (s.a.w):


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Wakati mmoja wenu atakapoamka akiwa amefunga, asitumie au asitoe lugha chafu na asifanye matendo maovu. Na kama yeyote yule anamchokoza au anagombana naye, hana budi kusema: 'Nimefunga, nimefunga.'



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 283


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

SIRI
Soma Zaidi...

MAANA NA FADHILA ZA DUA
DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Soma Zaidi...

Twahara
FIQH 1. Soma Zaidi...

Je! inajuzu wanawake kuzuru makaburi?
As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, nauliza inajuzu wanawake kuzuru makaburi? Soma Zaidi...

UKITAKA KUOMBA BASI MUOMBE ALLAH, UKIMKUMBUKA WAKATI WA RAHA ATAKUKUMBUKA WAKATI WA DHIKI, SHIDA NA TAABU
' ' ' ' ' ' ' ' ': "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': '... Soma Zaidi...

SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)
Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an. Soma Zaidi...

Namna ya kumvalisha sanda maiti, na kushona sanda ya maiti
Soma Zaidi...

Sababu za kushushwa kwa surat al-kafirum
SURATUL-KAFIRUN Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIM
Soma Zaidi...

KULA HALALI NA ZILICHO KIZURI NI AMRI KATIKA UISLAMU
' ' ' ' ' ' ': ' ' ' ' ' ' ' ' "' ' ' ' ' ' '... Soma Zaidi...

Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai
Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa. Soma Zaidi...