Kukaa itiqaf na sheria zake hasa katika mwezi wa ramadhani

Kukaa itiqaf na sheria zake hasa katika mwezi wa ramadhani

Kukaa Itiqaf



Kukaa Itiqaf katika kumi la mwisho la Ramadhani ni sunna iliyokokotezwa. Ki-lugha 'Itqaf' ina maana ya kukaa mahali. katika sheria ya Kiislamu 'Itiqaf' ni kukaa msikitini kwa ajili tu ya kumkumbuka na kumtukuza Allah (s.w) na kufanya ibada maalum kama vile kuswali, kusoma Qur-an na kufanya amali yoyote njema ambayo inaruhusiwa kufanyika msikitini nje ya shughuli za kawaida za kutafuta rizki. Kwa hiyo mahali pa kukalia 'Itiqaf' ni msikitini kama ilivyotajwa katika Qur-an:



'... Wala msichanganyike nao, na hali mmekaa Itiqaf misikitini .... ' (2:187).



Misikiti inayokaliwa Itiqaf iwe ni ile inayoswaliwa jamaa na Ijumaa ili pasiwe na haja ya kutoka kwa swala za jamaa au kwa swala ya Ijumaa. Wanawake wanaruhusiwa kufanyia Itiqaf zao majumbani mwao katika sehemu zao za kusalia lakini baada ya kupata ruhusa kutoka kwa waume zao. Kwa muda wote mtu atapokuwa katika Itiqaf haruhusiwi kutokatoka msikitini ila kwa dharura kubwa sana kama vile kwenda haja au kwenda kula. Mtu akiwa katika Itiqaf hulazimika kujitenga na shughuli zote za kutafuta maslahi ya maisha na shughuli zote za kijamii kama vile kutembelea wagonjwa, kuhudhuria mazishi, na kadhalika. Mtu anapokuwa katika Itiqaf haruhusiwi kuchanganyika na mkewe.


' ... Na w ala msichanganyike nao na hali mnakaa Itiqaf msikitini. (2:187).
Kwa ujumla katika muda huu wa kukaa Itiqaf, Mu'takif (Mwenye kukaa Itiqaf) anatakiwa ajihusishe tu na ibada maalum kama vile kuswali, kusoma Qur-an, kuleta tasbihi, tahmid, tahalili, takbir, istighfar na maombi mbali mbali.



Mu'takif anaruhusiwa kuja na matandiko yake msikitini na kuyaweka mahali pa uficho ambapo hayatawakarahisha watu wakati wa swala ya jamaa. Katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani mtu anaweza kukaa itiqaf kwa muda wowote ule, siku moja au masaa machache. Ni vyema mtu anapokuwa hana shughuli muhimu, anuie kukaa Itiqaf msikitini badala ya kujiingiza kwenye shughuli zisizo muhimu au shughuli za upuuzi zenye kumuingiza katika dhambi na kumpotezea muda ambao ni rasilimali pekee ya maisha yake. Katika mwezi wa Ramadhani Itiqaf imekokotezwa sana katika kumi la mwisho ili kumuwezesha Muumini kuudiriki usiku wa Lailatul-Qadr - akiwa katika hali ya kumkumbuka Allah (s.w). Mtume (s.a.w) alikuwa akikaa Itiqaf katika kumi hili la mwisho kama tunavyojifunza katika hadith zifu atazo:



Ames imulia Abdullah bin Umar (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akikaa Itiqaf katika siku kumi za mwisho za mw ezi wa Ram adhani. (Bukhari na Muslim).



Aysha (r.a.) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akikaa Itiqaf katika siku kumi za mwisho za Ramadhani mpaka alipotawafu (Allah alipo mchukua).Kisha wakeze waliendelea kukaa Itiqaf baada yake. (Bukhari na Muslim).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 204

Post zifazofanana:-

MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...

MAKTABA YA VIBABU KUTOKA BONGOCLASS
Soma Zaidi...

Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili
Soma Zaidi...

TEKNOLOJIA NA MAWASILIANO
Soma Zaidi...

Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE. Soma Zaidi...

Sababu kuu za maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, Tumbo la ngiri na chango
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kuulingania Uislamu kwa Jamii Yake
Nabii Ibrahim(a. Soma Zaidi...

sayansi
YALIYOMO1. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUTI
Soma Zaidi...

WAQFU WAL-IBTIDAAI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Nina vidonda kwenye uume wangu, je ni dalili ya nini?
Soma Zaidi...