lengo la kuswali za faradhi na suna

lengo la kuswali za faradhi na suna

Lengo la Kusimamisha Swala



Bila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Lengo la swala limebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo


'Soma uliyoletewa wahyi katika kitabu (Qur-an) na usimamishe swala. Bila shaka swala (ikiswaliwa vilivyo) humzuilia (mwenye kuswali na) mambo machafu na maovu, na kw a yakini kumbuko la Mw enyezi Mungu (lililomo ndani ya swala ni jambo) kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya). Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.' (29:45).



Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la kusimamisha swala ni kumtakasa mja na mambo machafu na maovu. Kwa maana nyingine, tunajifunza kuwa swala ikisimamishwa vilivyo, humfanya msimamishaji awe mtu mwema mwenye kutakasika na mambo machafu na maovu na mwenye kuendea kila kipengele chake cha maisha kwa kumtii Allah (s.w). Labda tujiulize swali: 'Ni nguvu gani au ni msukumo gani uliomo katika swala unaomfanya mwenye kuswali atakasike na maovu na awe na tabia njema anayoridhia Allah (s.w)' Linaloleta mabadiliko haya makubwa katika tabia na utendaji wa Muumini, ni lile kumbuko la Allah (s.w) lililomo ndani ya swala. Kwa hiyo lengo hili la swala litapatikana tu pale mwenye kuswali atakapokuwa na mazingatio na kumkumbuka Allah (s.w) katika kila hatua ya swala.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 171


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Vita vya Uhud na sababu ya kutokea kwake, Mafunzo ya Vita Vya Uhud
Vita vya Uhudi. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Bani Israil
Soma Zaidi...

kuwa na kauli njema, na faida zake katika jamii
11. Soma Zaidi...

Muhtasari wa sifa za waumini
Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s. Soma Zaidi...

Biashara haramu na njia zake katika uislamu
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...

nini maana ya hadathi na ni zipi aina za hadathi na uchafu katika uislamu
Soma Zaidi...

(xi)Hutoa Zakat na Sadakat
Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakat wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza. Soma Zaidi...

WAQFU WAL-IBTIDAAI
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Namna ya Kutayamam hatua kwa hatua, suna zake nguzo za kutayamam na masharti ya kutayamam
Soma Zaidi...

Ndoa ya mke zaidi ya mmoja na taratibu zake
Soma Zaidi...

HUKUMU ZA KUSOMA QURAN, HUKUMU ZA TAJWID, HUKUMU ZA NUN SAKINA, MIM SAKINA, QLQALA NA IQLAB, TANWIN NA MADA
Soma Zaidi...