Nyakati za swala za dharura swala ya mgonjwa na mafiri

Nyakati za swala za dharura swala ya mgonjwa na mafiri

Swala tano za Faradh katika Nyakati za Dharura



Amri ya kusimamisha swala tano imeambatana na nyakati makhususi kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


'Basi simamisheni swala Kwa hakika swala kwa waislamu ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi' (4:103)
Hivyo swala ya mja haitakubaliwa iwapo ataiswali nje ya wakati wake makhsusi. Hapana 'kadha' katika swala.



Pamoja na amri ya kuiswali kila swala ya faradhi katika wakati wake makhsusi, Allah (s.w) aliye Mwingi wa Rehma haikalifishi nafsi yoyote katika kuipa amri zake ila huitaraji kila nafsi itekeleze amri hizo kwa kadiri ya uwezo aliyoijaalia kuwa nao. Mara kwa mara katika kutufahamisha huruma zake juu yetu, Allah(s.w.) anakariri:



'Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila yaliyosawa na uwezo wake...' (2:286)
Baada ya kutoa ruhusa ya kutofunga wagonjwa na wasafiri, wakati wa mwezi wa Ramadhani na badala yake walipe 'kadha' siku walizokula anatudhihirishia Rehma zake kwa kutufahamisha:


'... Mw enyezi Mungu anakutakieni yaliyo m epesi, w ala hakutakieni yaliyo mazito...' (2:185)
Pia baada ya kutoa ruhusa ya kutayammam, baada ya kukosa maji, au kwa ajili ya maradhi au mtu anapokuwa safarini, katika Sura ya 5 aya ya 6, Allah (s.w) anamalizia kwa kusema:-


'... Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru'. (5:6)



'.. .Na ka m a m kiw a w agonjw a (mm eka tazw a ku tumia m aji) a u mm o safarini au mmoja wenu ametoka msalani (chooni) au mmewagusa(mmewajamii), wanawake - na msip ate maji basi ukusudieni (tayamamuni) udongo safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mw enyezi Mungu ni Mwenye kusamehe (na) Mw enye kughufiria '. (4:43)



'... Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi kusudieni (tayammamuni) udongo ulio safi na kuupaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru'. (5:6)



(2) Iwapo mgonjwa hajimudu na hana wa kumtwaharisha kwa maji au kwa udongo itabidi atayammamu kifikra na kuswali hivyo hivyo. Hili ni sahali kwa kauli ya Allah (s.w):


'Hapendi Allah kukutieni katika taabu, bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu'. (5:6)



(3)Mgonjwa anaruhusiwa kuswali akiwa amekaa na kuelekea Qibla iwapo ana uwezo huo, vinginevyo ataelekea popote pale kwa kadiri ya uwezo wake. Atarukuu na kusujudu katika hali hiyo ya kukaa iwapo anaweza, vinginevyo atarukuu na kusujudu kwa ishara tu.
(4)Iwapo mgonjwa hawezi hata kukaa ataswali akiwa amelala kwa ubavu huku akiwa ameelekea Qibla kama ana uwezo wa kufanya hivyo, vinginevyo ataelekea popote pale. Pia kama hawezi kulala kwa ubavu atalala chali. Kama hawezi kulala chali ataswali kwa ishara akiwa amelala vyovyote vile awezavyo.


(5) Pia mgonjwa anaruhusiwa kuchanganya swala kama msafiri (rejea swala ya msafiri) kama hivyo ndivyo hali ya mazingira ya ugonjwa inavyotaka.
Kutokana na tahfifu hizi, ugonjwa si udhuru wa kumruhusu mtu asiswali swala ya faradh kwa wakati wake hata kama mgonjwa huyo atakuwa mahututi kitandani akiwa nyumbani au hospitalini maadamu bado ana akili timamu.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 297


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Adabu ya kuingia katika nyumba za watu
Enyi mlioamini! Soma Zaidi...

HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Soma Zaidi...

Maharimu ni wanawake na wanaume walioharamishwa kuoana
Soma Zaidi...

Kitabu Cha Darsa za dua
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Zijuwe Suna zinazofungamana na swaumu na funga ya ramadhani
Soma Zaidi...

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII ADAM
Soma Zaidi...

Hatua ya Serikali Dhidi ya Waanzilishi wa Fitna na Farka wakati wa khalifa
Soma Zaidi...

namna ya kuswali swala ya msafiri, nguzo zake na hukumu zake
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? Soma Zaidi...

Vita vya Uhud na sababu ya kutokea kwake, Mafunzo ya Vita Vya Uhud
Vita vya Uhudi. Soma Zaidi...