Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

34.

Nini maana ya Husda, na ni yapi madhara yake

34. Kuepuka Husuda



Husuda ni miongoni mwa magonjwa makubwa ya moyo. Mtu mwenye husuda anadonda la chuki moyoni mwake juu ya neema alizoneemeshwa mwingine na Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa maana nyingine anachukia utaratibu wa Mwenyezi Mungu (s.w) aliouweka katika kugawanya neema zake kwa waja wake. Hasidi kutokana na chuki yake dhidi ya mja aliyeneemeshwa na Mwenyezi Mungu (s.w), huwa tayari kwa hali na mali kumdhuru mja huyo asiye na hatia yoyote. Ni kwa msingi huu Mwenyezi Mungu (s.w) anatufundisha kujikinga kwake na shari za viumbe vyake, akiwemo hasidi kama tunavyosoma katika Suratul-Falaq:


Sema: Ninajikinga na Mola wa Ulimwengu wote. Na shari ya alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo na shari ya wale wanaopulizia mafundoni na shari ya hasidi anapohusudu(1 13:1-5)



Husuda husababishwa na kutotosheka na kutoridhika na neema za Mwenyezi Mungu (s.w). Hasidi anataka kila neema aliyotunukiwa mwingine awe nayo yeye au mwingine abakie bila neema hiyo. Anataka awe juu ya mwingine na aonekane wa maana pekee katika jamii. Akihisi kuwa kuna yeyote aliyemzidi kwa cheo, utajiri, elimu, watoto,umaarufu, hupandwa na moto wa chuki moyoni mwake ambao humsukuma kufanya visa mbali mbali dhidi ya huyo anayemhisi kuwa amemzidi au yuko sawa n aye. Muislamu anatakiwa ajitakase na uovu huu wa husuda kwa kutosheka na kile alichonacho akijua kuwa kila neema aliyopewa mwanaadamu imekadiriwa na Mwenyezi Mungu (s.w). Na hapana yeyote mwenye uwezo wa kupunguza neema ya mtu aliyokadiriwa na Mola wake hata kwa kiasi cha chembe ndogo iliyoje na hakuna yeyote awezaye kumuongezea mtu neema kuliko vile alivyokadiriwa na Mwenyezi Mungu


(s.w).
Pia Muislamu wa kweli anajitahidi kujiepusha na husuda ili asije akaziunguza amali zake njema alizozitanguliza na akawa miongoni mwa watakaohasirika katika maisha ya akhera.



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: 'Kuweni waangalifu juu ya husuda, kwani husuda inaunguza amali njema za mtu kama moto unavyounguza kuni. (Abu Daud).



Husuda au wivu unaoruhusiwa ni ule unaofanywa kwa ajili ya kushindana katika kufanya mema. Wivu wa namna hii sio ule wa kuchukia kuwa kwa nini fulani ameneemeshwa bali ni ule unaomfanya mja ajitahidi zaidi kufanya mema kama anavyofanya au kumzidi mwingine. Mtume (s.a.w) ametufahamisha ni husuda ya namna gani inayoruhusiwa kwa Muislamu katika Hadithi ifuatayo:



Ibn Mas 'ud (r.a) am ehadithia kuw a Mtume w a Mw enyezi Mungu am esem a: Hapana husuda (inayoruhusiwa katika Uislamu) ila kwa watu wawili: 'Mtu ambaye Mwenyezi Mungu (s.w) amempa mali na akampa uwezo wa kuitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu na mtu ambaye Mwenyezi Mungu amempa elimu na hekima akawa anafundisha wengine pamoja na yeye mwenyewe kuingiza elimu hiyo katika vitendo'. (Bukhari na Muslim)




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 946


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

namna ya kuswali
11. Soma Zaidi...

UANDISHI WA HADITHI WAKATI WA TABI'INA
Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A. Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke Ulaya chini ya kanisa hapo zamani
Soma Zaidi...

JIFUNZE DINI YA KIISLAMU, quran, hadithi, tawhid, tajwid, sira na fiqh
Jifunze mengi kuhusu dini hapa Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII MUSA(A.S) NA HARUN(A.S)
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...

MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO
MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO. Soma Zaidi...

Kwa Nini Mwanaadamu Hawezi Kuunda Dini Sahihi ?
1. Soma Zaidi...

Ghasia na chokochoko za Makhawariji na kuuliwa kwa Ally
Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME DHUL-KIFL(A.S)
Mtume Dhul-kifl ananasibishwa na Ezekiel anayetajwa ndani ya Biblia. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kinyozi kaka wa kwanza
Soma Zaidi...

Imam Tirmidh na Jami'u At-Tirmidh
Soma Zaidi...

NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...