kuwa mwenye huruma na faida zake

25.

kuwa mwenye huruma na faida zake

25. Kuwa na Upendo



Upendo ni matunda ya vipengele vingi vya tabia njema vikiunganishwa pamoja. Kwa mfano kuongea na watu vizuri, kuwahurumia wakati wanamatatizo au kuwafanyia wema wa aina yoyote kama kuwasaidia kazi, kuwakirimu kitu n.k. ni miongoni mwa maadili mema yanayoleta upendo na mahusiano mema kati ya wanaadamu. Kinyume chake, kauli mbaya, ukatili, usengenyi, fitina, uchochezi, husuda, na matendo mengine mabaya kama haya yakitendwa kwa wan adam hujenga chuki na uadui.



Uislamu unatutaka tudumishe upendo kati yetu kwa kuwafanyia wenzetu mema tunayoyapenda na ambayo tungeliwataka wengine watufanyie. Pamoja na kusisitizwa na Uislamu kuwafanyia wengine mema na kujiepusha na kuwaudhi, tunashauriwa pia tuwe na tabia ya kupeana zawadi ili kukaza imara zaidi kifungo cha uhusianao mwema na upendo. Muislamu anashuriwa ajitahidi kutoa zawadi kuwapa wengine kila anapopata fursa ya kufanya hivyo na pia anashauriwa kupokea zawadi kwa moyo mkunjufu kila anapo pewa hata kama yeye ni tajiri na huyo anayempa ni maskini. Hebu turejee Hadith zifuatazo tuone jinsi Mtume (saw) anavyotuelekeza katika kupeana na kupokea zawadi:



Aysha(ra) amesimulai kuwa Mtume w a Allah amesema: Peaneni zawadi, kwani zawadi inaondoa chuki. (Tirmidh)
Aysha (ra) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akipokea zawadi akirudisha kitu kin gine badala yake kama badilisho kumpa yule aliyetoa. (Bukh ari).


Jab ir ames imulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yeyote yule aliyepewa zawadi na akawa na uwezo, na airudishie kwa zawadi nyingine , na yule ambaye hana kitu cha ku rejesha , na atoe shukurani na yule asiyetoa ahsante, ni mkosefu wa shukurani, na yule anayejifanya amepewa kitu na huku hakupewa, anakuwa kama yule aliyevaa magwanda(nguo) maw ili ya uw ongo ( ni mw ongo mkubw a-mnafiki). (Tirmidh, Abu-Daud).



Hadith hizi mbili zinatufahamisha kuwa zawadi isielekee upande mmoja tu bali kila anayepokea zawadi naye ajitahidi, kutoa zawadi ya namna nyingine kwa yule aliyempa kama ana uwezo na kama hana cha kutoa atoe ahsante na kumuombea dua aliye mzawadia.
Si tabia ya kiislamu kukataa zawadi- ya aina yoyote iliyohalali. Tunajifunza hili kutokana na hadith zifuatazo:



Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Ningalikaribishwa unyayo wa mguu wa mbuzi (uliopikwa) hakika ningalikaribia na ningalipewa zawadi ya mguu wa mbuzi, hakika ningali pokea. (Bukhari).
Anas amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa harudishi manukato yoyote (aliyopewa kama zawadi). (Bukhari)



Ibn Sayid amesimulia: 'Omar aliniteua kukusanya Zakat. Nilipo maliza na kuwasilisha zakat yote kwake, aliamuru nipwe ujira wangu. Nilisema: Nilifanya kwa ajili ya Allah na ujira wangu uko kwa Allah. Alisema: chukua kile ulichopewa kwa sababu niliteuliwa kufanya kazi kama hiyo wakati wa Mtume wa Allah. Aliniteua nikasema namna unavyosema. Mtume wa Allah akaniambia: unapopewa kitu ambacho hukukiomba, basi kula na toa sadaqa. (Abu Daud).



Hadith zote hizi zinatufundisha kuwa Muislamu akipewa kitu chochote cha halali asikatae hata kikiwa kidogo namna gani. Na kama hakihitajii sana, basi akipokee kisha atoe sadaqa. Pia tunapata fundisho kuwa Muislamu akikaribishwa na mwenziwe kula kitu chochote kilicho halali asikatae. Alimradi madhumuni ya kutoa na kupokea zawadi siku zote yawe ni kuzidisha upendo, udugu na mahusiano mema kati ya Waislamu na wanaadamu wote kwa ujumla.
Pia kutoleana salamu ni miongoni mwa nyenzo za kujenga upendo baina ya watu kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:


Abu Hurairah (ra) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema; 'Ham taingia Pep oni mpaka mw amini na hamtaamini mpaka mpendane. Je, nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu baina yenu' (Muslim)




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 137

Post zifazofanana:-

MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Soma Zaidi...

Dua Sehemu ya 02
Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa. Soma Zaidi...

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Soma Zaidi...

1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
1. Soma Zaidi...

ULCERS AND THEIR PROBLEMS
These occur as a result of the action of enzymes and acid on the epithelial membrane lining of the stomach and duodenum walls. Soma Zaidi...

Dawa ya kutibu mapunye
DAWA YA MAPUNYEMatibabu ya mapunye inategemea ni wapi mapunjye yapo. Soma Zaidi...

SABABU ZA KUKOSA HAMU YA TENDO LANDOA
Hii ni hali inayompata mtu kukosa hamu kabisa ya kushiriki kitendo chochote kinachohusiana na kufanya tendo landoa au bunyeto. Soma Zaidi...

Hoja juu ya hitajio la kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

Uchambuzi wa Neema Alizopewa Nabii Sulaiman(a.s)
(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake. Soma Zaidi...

'Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye'
Soma Zaidi...

Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani
Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV Soma Zaidi...