Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri

17.

Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri

17. Kuepuka kujisifu na kujitukuza


Waislamu tumekatazwa kujisifu sisi wenyewe na pia tumekatazwa kuwasifu wengine kupita kiasi.Mtume (saw) amekataza jambo hili katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (saw) amependekeza kwetu kuwa tumtupie mchanga (vumbi) usoni yule anayejihusisha na kuw asifus ifu w atu kupita kiw ango kinachos tahili. (Tirim idh).


Abu Bakar (ra) amesimulia kuwa mtu mmoja alimsifu mtu mwingine mbele ya Mtume (saw). Mtume (saw) alisema mara tatu. 'Ole wako umekata kichwa cha ndugu yako!' (Kisha anasema Mtume); Yeyote miongoni mwenu ambaye ataona hapana budi kumsifu mwingine na aseme; Nafikiri fulani yuko hivi na hivi ( ana sifa hizi na hizi) na Allah (sw) atamuhesabu hivyo kama kweli mbele yake anastahiki sifa hizo. Lakini asithubutu mtu kumpachika yeyote sifa ya Ucha-Mungu(wema) juu ya Allah.' (Bukhari na Muslim)
Aidha Allah (sw) ametukataza kujisifu sifu katika aya ifuatayo:

'Yeye (Allah) ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu; Yeye (Allah) anamjua sana aliyetakasika '. (53:32)


Kuwasifu sana watu kupita kiasi huwapelekea wale wenye kusifiwa kuvimba vichwa na kujihisi kuwa wao ni watukufu na bora zaidi kuliko wengine katika jamii. Tunayaona madhara makubwa yaliyojitokeza katika jamii ya waislamu kutokana na sifa za kupita kiasi tulizowapachika masheikhe zetu na watu wengine tuliowapachika usharifu, uwalii, ucha-mungu,n.k. Mgawanyiko wa waislamu tunaoushuhudia hivi leo kwenye madh-habu, twarika na matapo mengine mbali mbali, unatokana na dhambi hii ya kuwasifu viongozi wa hayo makundi kupita kiasi.


Pia tunajifunza katika historia kuwa chanzo cha Mitume wa Allah (sw) na watu wema kushirikishwa na Allah (s.w) ni kuwasifu kupita

kiasi. Katika Qur'an (9:30) tunafahamishwa kuwa kuwaiga washirikina waliowatangulia katika kuwasifu kupita kiasi viongozi wao, Mayahudi walimfaya Uzair (Mtu mwema) mwana wa Mungu na wakristo wakamfanya Isa Bin Maryam mwana wa Mungu. Kwa kuchelea watu wa Ummah nao wasijetumbukia kwenye shirki hii ya sifa, Mtume (saw) anatuasa katika Hadith ifuatayo:


' Imepokelewa kutoka kwa Umar(r.a) kuwa amesema Mtume wa Allah (saw) Msizidishe kwenye kunisifu kama walivyozidisha wakristo ( manasara) katika kums ifu mwana wa Maryam. Mimi ni mja wa Allah tu; kwa hiyo niiteni ;'Mja wa Allah na Mtume wake '. (Bukhari)
Hivyo muumini wa mkweli hanabudi kujiepusha na kujisifu sifu au kuwasifusifu watu. Na ikiwa hapana budi kumsifu mtu tuzingatie mipaka na tuseme kama alivyotuelekeza Mtume (saw) katika Hadith tuliyoirejea hapa juu. Tabia ya kujisifusifu au kuwasifusifu watu ni tabia ya uwongo, unafiki na ushirikina.



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 272

Post zifazofanana:-

Dalili kuu 7 za malaria na dawa ya kutibu malaria
Makala hii itazungumzia dalili za Malaria, athari za kuchelewa kutibu malaria, na matibabu ya malaria Soma Zaidi...

afya somo la 15
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Ni zipi funga za suna, na faida na fadhila zake pamoja na wakati wake wa kufunga
Soma Zaidi...

HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI
Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s. Soma Zaidi...

nataka niunganishe namba yangu kwa mtu mwingne ili kama kuna sms nimetumiwa ianzie kwa huyo mtu
Ikiwa nataka niunganishe namb yangu kwa mtu mwingne il kama kuna sms nime2miwa ianzie kwa huyo mtu nifanyeje? Soma Zaidi...

KITABU CHA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

SCIENTIFIC PROCESSES IN BIOLOGY
SCIENTIFIC PROCESSES IN BIOLOGYY THE USE OF SENSE ORGANS TO MAKE CORRECT OBSERVATION Sense organ this is an organ of the body that responds to external stimuli by conveying impulses to the sensory nervous system. Soma Zaidi...

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Pera
Soma Zaidi...

)Wenye kuepuka lagh-wi
Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Soma Zaidi...

DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...

Kitabu cha Afya 01
Soma kitabu hiki cha afya sehemu ya kwanza upate kuijua afya yako. Soma Zaidi...