Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa.

Presha ya kushuka (hypotension) dalili zake na njia ya kukabiliana nayo

RPESHA YA KUSHUKA (HYPOTENION)


Presha ya kushuka ama kitaalamu huitwa hypotension, presha ya kushuka ni hatari kwa afya kama ilivyo presha ya kupanda, maana mwili unakosa nguvu kabisa. Kama ilivyo presha ya kushuka presha ya kupanda unaweza kuizuia ana kujilinda nayo kwa kula vyakula salama.



VYAKULA MUJARABU KWA MWENYE PRESHA YA KUSHUKA


1.Tumia chumvi zaidi; wataalamu wa afya wanahimiza sana kutumia chumvi zaidi kwani madini ya sodium yaliyomo kwenye chumvi husaidia katika kupandisha presha. Ila tambua kuwa kwa wazee kuzidi kula chumvu kunaweza kusababisha moyo kujashinwa kufanya kazi vyema.
2.Kunywa maji mengi ya kutosha: maji husaidia katika kuongeza hali ya umajimaji kwenye miili. Hii husaidia kukabilia na upungufu wa maji mwilini (dehydration) hali hizi ni muhimu kwa kukabiliana na presha ya kushuka.
3.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kwa zaidi. Kwa mfano viazi mbatata, mchele na mikate
4.Kunywa chai yenye caffein;



DALILI ZA PRESHA YA KUSHUKA


1.Kushundwa kuona vyema
2.Kuchanganyikiwa
3.Kizunguzungu
4.Kuzimia
5.Uchovu wa hali ya juu.
6.Kuhisi baridi
7.Kushindwa kufikiri kwa kina
8.Kichefuchefu
9.Kushindwa kuhema vyema
10.Kutokwa na jasho




NJIA ZA KUKABILIANA NA MRESHA YA KUSHUKA


1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa muda wa dakika 30 mpka 60
2.Kunywa maji mengi na ya kutosha
3.Unapokaa usikae mkao wa kukunja miguu
4.Punguza ulaji wa vyakula vya wanga kama viazi mbatata, mchele na mikate
5.Punguza ama wach kabisa uvutaji wa sigara
6.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe.




HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA PRESHA YA KUSHUKA


1.Lala chini kwenye kitu kilicho flati.
2.Kunywa maji mengi
3.Tumia chumvi, unaweza kuilamba unaweza pia kukoroga chumvi kwenye kikombe na kunywa.
4.Kama hali inaendelea kuwa mbaya zaidi ni vyema kuwasiliana na kituo cha afya kilicho karibu nawe.



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1552


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-