Dalili (Alama) za Qiyama

Dalili (Alama) za Qiyama

Dalili (Alama) za Qiyama




Ingawa hakuna ajuaye Kiyama kitakuwa lini, kupitia Aya mbali mbali za Qur'an na Hadith kadhaa za Mtume (s.a.w) zinabainisha kwa uwazi juu ya dalili mbali mbali za kusimama kwa kiyama. Ziko Dalili kubwa na Dalili ndogo, na zipo ambazo tayari zimekwishadhihiri nyingine zinaendelea na ambazo bado kudhihiri kwake; Kama Allah Aliyetukuka anavyotubainishia:


'Kwani wanangoja jingine ila kiyama kiwajie kwa ghafla? Basi alama zake(hicho kiyama) zimekw ishakuja. Kutaw afaa w api kukumbuka wakati kitakapow ajia ? ' (47:18)
Pia anasema'Saa ya Kiyama imekaribia; na mwezi umepasuka' (54 :1)



Dalili Ndogo za Kiyama:




(i)Watu kumiliki mali na hali ya kuwa ni madhalimu wasio na uadilifu




(ii)Kuenea mno kwa riba kiasi cha kila mtu kuathiriwa nayo




(iii)Kuenea kwa kila aina ya Ulevi




(iv)Wanawake kukithiri katika kuvaa nguozinazochochea zinaa (nguo nyepesi za kuangaza , fupi na za kubana)




(v)Wanawake watawaiga wanaume katika mavazi kadhalika wanaume watawaiga wanawake katika mavazi. Leo wanaume wanavaa hereni, shanga, bangili, na mengineyo yanayojulikana kuwa mapambo ya kike.




(vi)Kuenea kwa Liwati (kujimai baina ya jinsia moja-wanaume kuwaendea wanaume wenzao na wanawake kuwaendea wanawake wenzao) Homosexuality and Lesbiansm. Jambo hili leo limehalalishwa na watu wa Magharibi, pia hapa kwetu Afrika na hasa Kenya na Afrika kusini ni halali Mwanaume kuolewa na mwanamume mwenzake! Subhaanallah!




(vii)Kuenea sana kwa zinaa na itafanyika hadharani.




(viii)Watu hawatawajali tena wazazi wao, ndugu zao najamaa zao badala yake watawathamini nakuwasaidia rafiki zao.




(ix)Watu watachukia sana kulea watoto.




(x)Unafiki utaenea sana.




(xi)Mauaji yataenea sana, kwa kutoka Taifa mojakwenda kulivamia Taifa jingine na watu baadhikuwaua wengine kwa maslahi yao binafsi




(xii)Watu wataona uzito sana kutoa sadaka




xiii)Watawala watakuwa wengi sana lakini hakuna atakayekuwa mkweli na mwadilifu




xiv)Mtu ataheshimiwa kwa shari yake na si kwa uadilifu na wema wake.




xv)Kujifaharisha kwa misikiti




xvi)Pamoja na haya yote, bado kutakuwepo na kundi dogo tu la waislamu ambalo litadumu katika njia iliyonyooka na halitatetereka kwa lolote.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 394


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Ujuwe utaratibu mzima wa funga na kutekeleza ibada ya Swaumu
Soma Zaidi...

Mifumo ya benk na uchumi wa kiislamu
7. Soma Zaidi...

Khalifa na Uendeshaji wa Dola kwa ujumla, kulinda wasio waislamu na haki zao na mali zao.
Soma Zaidi...

Nyakati za swala za dharura swala ya mgonjwa na mafiri
Soma Zaidi...

ihram na nia ya Hija na Umra
1. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SHUAIB
Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU
Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Soma Zaidi...

Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...

Kushuka na kuhifadhiwa kwa quran, hatua kwa hatua: mafunzo ya baadhi ya sura za quran
QUR'AN 5. Soma Zaidi...

Sheria Katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Haki za kiuchumi za mwanamke katika uislamu
Haki za UchumiKuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii. Soma Zaidi...