namna quran inavyogawanya mirathi na wanaorithi pamoja na mafungu yao

Qur-an inavyogawa MirathiMgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.

namna quran inavyogawanya mirathi na wanaorithi pamoja na mafungu yao

Qur-an inavyogawa Mirathi
Mgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni (wawili au) zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili (2/3) ya mali aliyoiacha (maiti,).



Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi apewe nusu. Na wazazi wake wawili kila mmoja wao apate sudusi (1/6)ya mali aliyoiacha (maiti), akiwa maiti huyo (anaye mtoto au mjukuu). Lakini kama hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake basi mama yake atapata (1/3,)(na baba) thuluthi mbili (2/3,). Na kama (huyo maiti) anaye ndugu basi mama yake atapatya sudusi moja (1/6). Na huku kurithi kunakuwa baada ya kutoa aliyoyausia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyingi hamjui ni nani miongoni mwao aliye karibu zaidi kukunufaisheni. Hiyo ni sheria iliotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mjuzi mwenye hikima. (4:11)



Na nyinyi mtapata nusu (1/2) ya (mali) walizoacha wake zenu, kama wao hawana watoto (wala wajukuu). Na ikiwa wana mtoto (au mjukuu), nyinyi mtapata robo (1/4) ya
walivyoviacha, baada ya kutoa walivyousia au kulipa deni. Nao (wake zenu watapata robo ya mlivyoviacha, ikiwa hamna mtoto (wala mjukuu) basi wao (hao wanawake) watapata thumni (1/s) ya vile mlivyoviacha, baada ya kutoa mlivyousia au kulipa deni. Na kama mwanamume au mwanamke ni mkiwa - hana mtoto (wala mjukuu) wala wazazi, lakini anaye kaka *('wa kwa mama) au dada (wa kwa mama pia), basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi (sehemu ya sita). Na wakiwa zaidi kuliko hivyo basi watashirikiana katika thuluthi baada ya kutoa vilivyousiwa au kulipa deni, pasipo kuleta dhara. (Huu) ndio wasia uliotoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye Upole. (4:12)



Wanakuuliza sema: 'Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Kama mtu amekufa, hali hana mtoto, lakini anaye dada; basi atapata (huyo dada) nusu ya yale aliyoyaacha (maiti). Na yeye (mtu huyu) atamrithi (dada yake) ikiwa hana mwana. Na kama wao ni (madada) wawili, basi watapata thuluthi mbili za yale aliyoyaacha. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi (kila) mwanamume (mmoja) atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni iii msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu. (4:176)



Kama ilivyosisitizwa mwishoni mwa aya hizi, huu ndio mgawanyo wa mirathi aliouweka AIah (s.w) na kugawanya mirathi kwa kufuata sheria ya kimila, sheria ya Bunge au sheria nyingine yoyote ya kitwaghuuti, ni kuchupa mipaka ya Mwenyezi Mungu. Allah (s.w) anasisitiza kufuatwa kwa sheria hii katika aya mbili zinazofuatia hizi:


Katika aya hizi zinazobainisha mgawanyo wa mirathi (4:11-12), (4:176) tunajifunza kuwa watoto wa kiume/wanaume wanapata mara mbili ya watoto wa kike/wanawake na baba anapata mara mbili zaidi kuliko mama. Je, sheria ya Allah (s.w) inapendelea wengine na kuwadhulumu wengine haki zao? Allah (s.w) ni Mkwasi, Mwenye kujitosheleza asiyehitajia chochote kutoka kwa viumbe vyake, bali viumbe ndio wanaomuhitajia. Pia Allah (s.w) ni Muadilifu na mpole mno kwa viumbe vyake. Hivyo, Allah (s.w) ametakasika na kila sifa mbaya na kila sifa za upungufu kama vile kupendelea au kudhulumu baadhi ya viumbe vyake. Kwa vyovyote vile, mgawanyo huu wa Allah (s.w) ni mgawanyo unaotoa haki kwa kila mrithi kwani ni mgawanyo wa mjuzi, mwenye hikima na mpole kwa viumbe vyake. Mwenyezi Allah (s.w) amemalizia aya hizi kwa msitizo:


"...Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mjuzi na mwenye hi/dma." (4:11).


Huu ndio usia uliotoka kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni mjuzi na mpole. ". (4:12).


"... Mwenyezi Mungu anakubainishieni iii msipotee; na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu." (4:176).


Kwa kuzingatia majukumu ya wanaume na wanawake katika familia, kuna hekima kubwa ya kumzidishia mwanamume mara mbili ya kile anachopata mwanamke katika mafungu ya mirathi. Mwanamke amepunguziwa fungu kwa kuwa hana matumizi ya kumlazimu kama alivyo mwanamume. Halazimiki kwa matumizi ya watoto wake, na kazi yake na hata matumizi yake binafsi.



Bali matumizi yote hayo huwa juu ya mwanamume. Kwa mfano, iwapo urithi ulioachwa na baba mzazi kwa mtoto wake wa kike na wa kiume ni shilingi 3,000,0001=, kulingana na mgawanyo wa Qur-an mtoto wa kiume atapata shilingi 2,000,000/= na mtoto wa kike atapata shilingi 1,000,000.



Utakuta zile za kijana mwanamume zitakwisha kwa matumizi mbali mbali yanayomlazimu ikiwa ni pamoja na matumizi ya huyo dada yake ambaye licha ya kutowajibika kutoa matumizi kwa yeyote yeye mwenyewe anabakia kutunzwa na kulelewa na kaka yake na yuko huru kutumia urithi wake huo hata kwa kununulia mapambo ya dhahabu.
Mwanamume amezidishiwa fungu kwa sababu matumizi yake yanayomlazimu kisheria ni mengi. Ndiye mwenye jukumu Ia kugharamia gharama zote za maisha kwa mke wake/wake zake na watoto wake, wazazi wake na wale wote wanaomtegemea katika familia.



Bila shaka, wale wanaoishutumu sheria hii ya mirathi kuwa inawakandamiza wanawake, hawajaiona hekima hii au wamepata mwanya wa kuwaghilibu watu waone sheria zilizotungwa na mwanaadamu ndizo bora kuliko sheria ya Allah (s.w). Allah (s.w) anatutanabahisha:


Je, wao wanataka hukumu za kijahili? Na nani aliye mwema zaidi katika hukumu kuliko Mwenyezi Mungu, kwa watu wenye yakini? (5:50).
Aya tulizozirejea (4:11-12) na (4:176) zimetaja kwa uwazi na kwa ukamilifu watu wenye kurithi na mafungu yanayorithiwa.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 198

Post zifazofanana:-

MATIBABU YA FANGASI
Karibia fangasi wote hawa wanatibika bila ya ugumu wowote maka mgonjwa atakamilisha dozi. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Tikiti
Soma Zaidi...

maktaba
Soma Zaidi...

BINTI MZURI ASIYETAMBULIKA
BINTI HUYU NI NANI? Soma Zaidi...

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...

HADITHI YA MWEN YEKUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITI YA MWENYE KUTABIRIWA MTOTO WA TAJIRI Kwanza tambua ewe ndugu yangu kuwa mimi ni mtoto wa tajiri mkubwa sana katika nchi yetu hii. Soma Zaidi...

KAMA HUNA HAYA BASI FAJA UNACHOTAKA
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ' ' ' ' ' '?... Soma Zaidi...

HADITHI YA TABIBU NA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA TABIBU WA MFALME Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 40: Kuwa Duniani Kama Vile Mgeni Au Mpita Njia
Soma Zaidi...

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA
*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko. Soma Zaidi...

DUA ZA WAKATI WA HASIRA
DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA. Soma Zaidi...

Upungufu wa vitamini C na dalili zake mwilini
makala Soma Zaidi...