Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kiafrika hapo zamani

3.

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za kiafrika hapo zamani

3. JAMII ZA KIAFRIKA



Katika bara Ia Afrika pamoja na kuwa na jamii nyingi zenye mila na desturi zinazotofautiana hatupati hata jamii moja ya kitwaghuti iliyompa mwanamke sauti katika nyumba wala katika jamii. Matatizo au makosa yote yaliyofnayika nyumbani yalisukumizwa kwa mwanamke. Mwanamke alifanyishwa kazi na kubebeshwa mizigo kama punda. Mwanamke hakuwa na haki ya kumiliki mali aliyoichuma mwenyewe. Kutokana na mahari yaliyolipwa wakati wa kuolewa mwanamke alifanywa mali ya mumewe ambaye aliweza kumfanya lolote alitakalo kama anavyofanyiwa mtumwa.


Pia katika jamii nyingi za Kiafrika, situ kwamba mwanamke hakuwa na haki ya urithi bali yeye mwenyewe alirithiwa kwa nguvu na mmoja wa shemeji zake. Akili ya mwanamke katika jamii nyingi imelinganishwa na ile ya mtoto mdogo. Kwa sababu hii mwanamke hakutakiwa ushauri kwa jambo lolote lile katika familia. Mara nyingi ushauru wa mtoto wa kiume ulithaminiwa kuliko ule wa mama yake. Kwa ujumla katika jamii nyingi za Kiafrika mwanamke alidunishwa kwa kiasi kikubwa.


Pamoja na kazi kubwa ya uzazi na malezi ya watoto, mwanamke aliachiwa majukumu yote ya nyumbani na alikuwa mshiriki mkuu katika shughuli za uchumi ambapo mali aliyoichuma kwa jasho lake ilichukuliwa na mwanamume bila hata kushauriwa. Hivi ndivyo alivyo nyanyaswa na kudunishwa mwanamke katika jamii mbali mbali za ulimwengu katika nyakati mbali mbali za historia. Je hivi leo zimechukuliwa hatua gani ili kukomesha uonevu huu dhidi ya mwanamke?



Katika miaka hii pamekuwa na vuguvugu Ia kumkomboa mwanamke ili kumrudishia haki zake na hadhi yake iliyodhulumiwa na wanaume. Vyama vingi vya kisiasa vimelipa suala hili kipa umbele na vimeundwa vyama vya wanawake vya Kitaifa na Kimataifa vinavyojishughulisha tu na kumkomboa mwanamke. Je, vyama hivi vimeleta mafanikio yoyote?


Ukichunguza mbinu zinazotumiwa na vyama hivi katika ukombozi huu wa mwanamke, utakuta hazina tofauti kabisa na zile zilizotumiwa na Ulaya na Marekani katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda za kumtaka mwanamke.



(a)Awe sawa na mwanamume kwa kila kitu bila ya kuzingatia tofauti za kimaumbile na nafasi ya mwanamke na mwanamume katika jamii.
(b)Ashiriki sawa na mwanamume katika uchumi na siasa na kumfanya ajitegemee kiuchumi.
(c)Awe huru kutoka nyumbani kwake na kuchanganyika na wanaume apendavyo.



Tuliona kuwa, matokeo ya kumtetea mwanamke kwa mtazamo huu haikuwa kumkomboa bali kumdhalilisha zaidi na kumvua haya na utu wake. Pia ukombozi wa mwanamke kwa mtazamo huu haukuleta nafuu yoyote katika jamii bali umezidi kuidumaza na kuigharimu kiasi kikubwa. Kampeni hii ya ukombozi wa mwanamke imechangia sana katika kuvunja maisha ya familia na kueneza magonjwa ya zinaa na kuongeza idadi ya wavuta bangi, wazururaji na majambazi kaitka jamii.



Ni nani hasa aliyemkombozi wa mwanamke? Bila shaka ni yule aliyemuumba na kumleta hapaduniani kama mwenza wa mwanamume. Hivyo haki na hadhi ya mwanamke itapatikana kwa kumuamini Allah (s.w) na kufuata muongozo wa maisha aliouweka katika kukiendea kila kipengele cha maisha ya binafsi, familia.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 99

Post zifazofanana:-

Zijuwe Faida za Kuwa na Istiqama (Msimamo Thabiti)
38. Soma Zaidi...

Asteroids, Meteorites, Comets and Satellites
These are solid metal rock objects that orbit the sun, and they are not as bigger as planets. They are mostly found between the orbit of Mars and Jupiter. Soma Zaidi...

maradhi
Soma Zaidi...

SIRI
Baada ya kutulia vizuri unaanza kukumbuka umefikaje hapa kwenye misitu. Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA MTUME IDRISA (A.S)
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a. Soma Zaidi...

MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO
MAANA YA ZAKA NA SADAKA KULUNGA NA KISHERIA PAMOJA NA TOFAUTI ZAO. Soma Zaidi...

ALAMA YA MUUMINI WA UKWELI KATIKA UISLAMU
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': "' ' ' ' '... Soma Zaidi...

UMBILE LA MBINGU NA ARDHI
'Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s. Soma Zaidi...

DUA 61 - 84
61. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA (sehemu ya kwanza): KIAPO CHA SULTAN
Soma Zaidi...

Kuangamizwa Firauni na Majeshi Yake
Soma Zaidi...

Dalili 10 za kukaribia kujifungua pamoja na uchungu wa kujifungua
Download Kitabu cha elimu ya Ujauzito na malezi ya mimba. Soma Zaidi...